Mwanamasumbwi wa uzito wa juu Tyson Fury baada ya kupata ushindi wa “Knock Out” dhidi ya Dillian Whyte na kutetea ubingwa wake wa ‘WBC heavyweight’ na kusema kuwa imetosha sasa na anatundika glovu kwenye mchezo huo.

Tyson Fury ameweza kutetea ubingwa wake na kulinda rekodi yake ya kupigana mapambano 33 pasipo kupoteza hata pambano moja, huku akishinda mapambano 32 na kutoa sare pambano 1,  baada ya kumtandika mwingereza mwenzie kwa KO kwenye raoundi ya sita kwenye uwanja wa Wembley.

Tyson Fury amemchakaza Wladimir Klitschko ambaye alishikilia nafasi ya kuwa bingwa wa dunia kwa muda mrefu, na kwa sasa Fury anachukuliwa kama ni mwanamasumbwi bora wa kisasa katika kipindi hiki.

Kwa sasa Fury haoneshi kuvutiwa na kupigana na Oleksandr Usyk ambaye anashikilia mikanda ya WBA, IBF na WBO, wala muingereza mwenzie Anthony Joshua na badala yake amesisitiza kuwa anataka kustaafu tu.

“Nimejitoa kwenye ngumi kwa miaka 20,  kwenye mapambano ya ridhaa na ya kulipwa, nimepigwa kichwani, nimeangushwa chini na nimekuwa na mapambano magumu, nimetoa sare, nimeshinda na nimepigana karibia dunia nzima.” Alisema Fury.

“Ni kiasi gani ynaweza kupata kwenye jiwe? nimetoa kila kitu na kukiweka kwenye mstari kila muda niliopata na sasa imetosha. Ikiwa ni swala la pesa ningeendelea lakini sio kuhusu pesa, na nina furaha.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa