Wardley Bado Hajakata Tamaa Baada Ya Kipigo Kizito

Fabio Wardley amepitia usiku mgumu zaidi katika maisha yake ya ngumi baada ya kupoteza pambano lake la kwanza kabisa la kulipwa dhidi ya Daniel Dubois, pambano lililoandika historia kwa ubabe, damu na mapambano makali ndani ya ulingo.

Wardley Bado Hajakata Tamaa Baada Ya Kipigo Kizito

Mbali na kupoteza mkanda wa WBO uzito wa juu, Wardley pia alipoteza nafasi ya kuwania pambano kubwa dhidi ya bingwa Oleksandr Usyk. Lakini kilichoumiza zaidi ni namna alivyopokea adhabu kubwa kutoka kwa Dubois katika raundi za mwisho, kabla ya refa kusimamisha pambano kwenye raundi ya 11.

Cha kushangaza, licha ya kipigo hicho, Wardley bado alionyesha moyo wa kishujaa baada ya pambano. Kupitia ujumbe wake, bondia huyo alisema: “Mwili wangu umeshindwa, lakini moyo wangu haujashindwa.” Kauli hiyo imewavutia mashabiki wengi walioguswa na namna alivyopambana hadi mwisho licha ya mateso aliyopitia ulingoni.

Wardley Bado Hajakata Tamaa Baada Ya Kipigo Kizito

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Pambano lilianza kwa kasi ya ajabu ambapo Wardley alimwangusha Dubois ndani ya sekunde 10 za mwanzo kabisa na tena katika raundi ya tatu, jambo lililoonekana kuwapa mashabiki matumaini ya ushindi mkubwa. Lakini baada ya hapo, Dubois aligeuka mnyama ndani ya ringi na kuutawala mchezo kwa nguvu, mashambulizi na usahihi mkubwa wa ngumi zake.

Wardley Bado Hajakata Tamaa Baada Ya Kipigo Kizito

Takwimu zilionyesha tofauti kubwa ya ubora ndani ya pambano hilo, huku Dubois akipiga ngumi nyingi zaidi na kwa usahihi mkubwa kuliko Wardley. Sasa rekodi ya Wardley imesimama kwenye ushindi 19, sare moja na kipigo kimoja, huku Dubois akiendelea kujijengea heshima kubwa katika uzito wa juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.