Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Chama cha Ngumi Mkoa wa Tanga waadhimisha siku ya kimataifa ya Ngumi Duniani (27 August) katika Jiji la Tanga.
Makamu wa Raisi wa BFT nchini Tanzania na Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Nassor Abbas Makau aliongoza maadhimisho hayo Jijini Tanga siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya Klabu Bingwa ya Taifa.Maadhimisho ya siku hii muhimu ya ngumi kimataifa chini ya IBA (International Boxing Association) yalihudhuriwa na mabondia wengi kutoka Mkoa wa Tanga huku kauli mbiu ikiwa ni #himiza #elimisha #kuhamasisha jamii yetu. “Tunahimiza kila mtu kuwa na mazoea ya mchezo wa ngumi katika siku hii ya kumbukumbu ya ngumi Duniani” #NGUMIKILAMAHALI #BOXINGEVERYWHERE
Washiriki walifanya mazoezi ya pamoja ya viungo na mapigo huru na kivuli ya ngumi (Shadow box) katika uwanja wa Mkwakwani.
Katibu Mkuu wa BFT Tanzania Ndg. Makore Mashaga alikua mratibu mkuu wa shughuli hio.