Kuelekea August 14, 2021. Deontay Wilder ameingia kwenye mpango wa pambano la Tyson Fury vs Anthony Joshua (AJ), mashaka yaibuka kuelekea pambano la “All British”.

Imeripotiwa kuwa, Fury ameelekezwa kupambana na Wilder kwa mara ya 3 kabla ya kuingia ulingoni kuchuana na AJ. Pambano la Fury na AJ ni pambano kubwa linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa ndondi duniani. Huu ni mpambano ambapo mataji yote manne yatawekwa mezani na bingwa atayachukua yote na kuwa bingwa wa dunia.

Itakumbukwa, Februari 2020 Fury alishinda mkanda wa WBC kwenye mchezo wa marudio ambao alimzidi nguvu Deontay na kulikuwa na makubaliano kuwa wawili hawa wangepambana kwa mara ya 3.

Pambano la mara ya tatu kati ya Fury vs Deontay lilichelewa baada ya kuenea kwa maambikizi ya Covid19 na hivyo baada ya muda, Fury alisema ataendelea na mambo mengine na kuachana na pambano hilo.

Mambo yamekuwa tofauti, Deontay aliamua kuchukua uamuzi wa kimahama katika kutafuta suluhisho na pambano lake dhidi ya Fury lilisogezwa mpaka 2021 kitu ambacho Fury alikikataa toka awali.

Baada ya taratibu za kimahakama, Jaji Daniel Weinstein ameweka siku ya mwisho kwa pambano la Fury vs Deontay kufanyika. Tarehe yeyote itayopangwa, isizidi Septemba 15 na hivyo Fury amepewa sharti la kumalizana na Wilder kabla ya kuchuana na Anthony Joshua.

Hakika vita ya kumsaka bingwa wa dunia inashika kasi!


Unaweza kuwa milionea wakati wowote!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Wilder, Wilder Aingilia Kati Pambano la Fury vs AJ, MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa