Kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers amesema hana mpango wa kuzungumza kuhamia Tottenham kwa sasa kwa kuwa anaamini timu yake ipo katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano mikubwa.

Rodgers amekuwa akihusishwa na kujiunga na Spurs baada ya Jose Mourinho kutimuliwa wiki iliyopita, wakati kocha wa muda Ryan Mason akichukua mikoba hiyo mpaka mwisho wa msimu.

 

Brendan Rodgers

Tetesi hizo zimetapakaa zaidi baada ya kocha aliyekuwa akipigiwa upatu zaidi, Julian Nagelsmann kuamua kujiunga na mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.

Alipoulizwa kuhusu tetesi za yeye kujiunga na Spurs, Rodgers alisema: “Tottenham ni klabu bora, moja ya klabu kubwa nchini, kubwa sana. Lakini mtazamo wangu upo hapa.

“Nipo katika moja ya kituo bora cha michezo duniani, mradi tulionao hapa, bado tunataka kuukuza, bado tuna kazi nyingi za kufanya hapa.

“Nina uhusiano mkubwa na wachezaji na bodi, na tuna mipango ya kuendelea kusonga mbele.”

Leicester City walitaka kumaliza Primia Ligi katika nafasi nne za juu msimu uliopita lakini ushindi mara 3 katika michezo yao 14 ya mwisho ilimfanya Rodgers kupoteza nafasi hiyo katika siku za mwisho za kampeni.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa