Nyota wa Manchester United Bruno Fernandes ameeleza kwamba anamkubali kiungo mwenzake wa timu hiyo Paul Pogba.

Katika mahojiano na kipindi kimoja cha televisheni, Bruno alieleza namna ambavyo wamejiuana na Pogba toka alivyokuwa Juventus ya Italy na kiwango kikubwa ambacho wawili hao wanacheza kwa kushirikiana kiwanjani.

Bruno alieleza namna ambavyo mabeki na wachezaji wa timu pinzani wanavyopata wakati mgumu kipindi wanapokutana na wachezaji wawili wanaoweza kucheza na mpira ipasavyo. Pogba alionekana kupoteza furaha yake katika timu ya Manchester United kipindi cha nyuma lakini siku za hivi karibuni ameonekana kupenda kusakata kabumbu akiwa na mashetani hao wekundu wa manchester.

Nahisi Paul ni miongoni mwa wachezaji bora duniani hivi sasa,na huwa anatoa ushauri kwa wenzake muda kwenye vyumba vya kubadili nguo. Ni mcheshi sana” Alisema Fernandes.

Kwangu mimi, kucheza na Paul kunanifanya nioneshe uwezo mkubwa. Kucheza na mtu anayejua kunanifanya nifanye mazuri zaidi na nahisi hilo limenifanya kuonesha uwezo mkubwa sana napokuw kiwanjani.” Alimalizia Bruno.

Bruno Fernandez amekuwa ni mchezaji tegemewa wa Manchester United toka asajiliwe klabuni, akiwa amecheza michezo 32 ya EPL na kufunga magoli 16 NA akitoa pasi 11 za magoli. Akasekanapo kwenye kikosi kinachoanza cha Manchester United, basi mashabiki wa timu hiyo uwaza sana.

Bado haijajulikana kama Pogba ataendelea kuchezea Manchester United, lakini naamini kuwa Bruno na mashetano hao watatamani ataendelea kuhudumu manchester United na kusaidia kufikia malengo ya klabu.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

bruno, Bruno Fernandez Anamkubali Pogba, Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa