Afisa habari wa bodi ya ligi Tanzania maarufu kama NBC Karim Boimanda amezungumza na kutoa tathmini juu ya mwenendo wa ligi kuu Tanzania Bara.
Afisa huyo wa habari ameeleza asilimia 80 ya ya michezo ya mizunguko miwili iliopigwa ilipigwa katika viwanja vyenye hadhi ya kutumika katika ligi kuu Tanzania.
Ameeleza mpaka kufikia mzunguko wa pili ni kiwanja kimoja tu ndicho kiligundulika hakina ubora wa kutumika nacho ni kiwanja Highland estate kinachotumika na klabu ya jijini Mbeya.
Huku akieleza viwanja ambavyo vilifungiwa hapo mwanzo vinapaswa kukaguliwa tena na wakaguzi ili viweze kuthibitika kwa matumizi tena na viwanja hivyo ni pamoja na Mkwakwani uwanja unaotumika na klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga pia kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma kinachotumika na klabu ya Dodoma Jiji.
Boimanda amesisitiza wamejitahidi sana kwenye usimamizi wa viwanja na kuhakikisha michezo inachezwa katika viwanja vinakidhi matakwa ya kanuni za bodi ya ligi.