Usiku wa leo itashuhudiwa fainali ya CAF Super Cup kati ya Al Ahly ya Misri dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

CAF Super Cup ni kombe ambalo huchezwa kila mwaka Afrika ambako mshindi wa Kombe la mabingwa Afrika anacheza na mshindi wa kombe la shirikisho. Mwaka jana, Al Ahly ilishinda kombe la Afrika na RS Berkane ikashinda kombe la shirikisho hivyo wawili hao watakutana leo ili kutambua mshindi.

Kocha wa Al Ahly, Pitso Misomane ameeleza kuwa anawaheshimu sana RS Berkane na anaamini ni kikosi kilichokuwa bora sana na hawezi kuwadharau.

Mosimane pia ameeleza kuwa safari ndefu zinazotokana na kushiriki michuano mingi inaweza kuwatoa kwenye reli na kuona kuwa RS Berkane wapo kwenye nafasi nzuri zaidi lakini kwa kuwa CAF Super Cup ni kombe kubwa litawapa motisha na watafanya poa sana.

“Berkane ni timu nzuri na yenye nguvu na tunaamini itatupa changamoto kubwa uwanjani. Na ni kweli ukiwa kocha wa Al Ahly, kila mchezo unakuwa na presha kubwa na si uongo tunahitaji makombe zaidi na hili la CAF Super Cup ni mojawapo tu hivyo tutafanya kazi tuwezavyo kubeba kombe hili. Tutalitafuta kombe mpaka tulipate”, alimalizia Mosimane.

Fainali ya kombe hili la CAF Super Cup ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1993. Toka hapo ni Al Ahly ndio timu iliyoshinda mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote ikifanya hivyo mara 6 kati ya 8 iliyocheza fainali hizo.

BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa