Simba leo itajitupa na klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana huko nchini Sudani kwenye mchezo wa kirafiki baada ya kupisha michuano ya kimataifa.

Simba

Wekundu hao wa msimbazi ambao walifika juzi nchini Sudani kwajili ya kushiriki michuano maalumu waliyoalikwa na klabu ya Al Hilal ya nchini humo ambayo watatumia mechi hizo kama sehemu ya kujipima kuelekea michuano ya kimataifa itakayoanza mapema mwezi wa tisa.

Klabu ya Simba baada ya kumaliza michuano hiyo nchini Sudani itarejea kumalizia michezo yake ya kirafiki dhidi ya klabu ya Arta Solar ya nchini Djibouti na michezo yote ni maalumu kwajili ya kujipima nguvu na kujiimarisha kwajili ya mechi za kimashindano.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa