Aishi Manula Arejea Kikosi cha Taifa Stars Kujiandaa na Michezo ya FIFA Series 2026

Golikipa wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosicha taifa stars  kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki ya FIFA Series 2026 itakayofanyika Rwanda. Taifa Stars itacheza mechi hizo Machi 26 na Machi 29, 2026, huku wachezaji wakiwajibika kuanza kambi ya mazoezi kuanzia Machi 22.

Aishi Manula Arejea Kikosi cha Taifa Stars Kujiandaa na Michezo ya FIFA Series 2026Kikosi cha wachezaji 25 kilichotangazwa na kocha Miguel Ángel Gamondi kina mchanganyiko wa wachezaji wa ndani na wachezaji waliopo klabu za kimataifa. Mbali na Manula, golikipa wengine walioitwa ni Yona Amosi kutoka Pamba Jiji na Zuberi Foba wa Azam FC.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kati ya wachezaji walioitwa, kuna wachezaji mashuhuri kama Haji Mnoga kutoka Salford City, ya Uingereza, Novatus Dismas kutoka Göztepe FC, Uturuki, Alphonce Mabila kutoka Shamakhi, Azerbaijan, na Charles M’Mombwa kutokea Floriana FC, Malta, wakionyesha mchanganyiko wa ubora na uzoefu wa kimataifa ndani ya kikosi.

Aishi Manula Arejea Kikosi cha Taifa Stars Kujiandaa na Michezo ya FIFA Series 2026Wachezaji wengine waliotajwa ni pamoja na Nickson Kibabage wa Simba SC, Bakari Mwamnyeto Yanga sc, Mohamed Hussein Yanga sc  Ibrahim Abdulla Yanga sc, na wengine, wote wakiwa wamechaguliwa kwa uwezo wao wa kipekee na mchango wanayoweza kuleta katika timu.

Aishi Manula Arejea Kikosi cha Taifa Stars Kujiandaa na Michezo ya FIFA Series 2026Maandalizi haya ya kikosi cha Taifa Stars yanatarajiwa kuhakikisha timu inakuwa tayari kushindana kikamilifu kwenye michezo ya kimataifa kirafiki ya FIFA Series 2026.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.