Algeria wameanza kampeni yao ya TotalEnergies CAF Women’s Africa Cup of Nations Morocco 2026 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Senegal kwenye mechi ya ufunguzi ya Kundi A mjini Rabat.

Magoli ya Ushindi yalifungwa dakika ya 13 ambapo Marine Dafeur alifunga kwa penalti, akitoa uongozi wa mapema. Dakika ya 85 Mélissa Bethi akamaliza kwa ustadi baada ya pasi ya Lina Boussaha, akihakikisha pointi tatu muhimu.
Katika mchezo huo uliokua na mvuto wa hali ya juu, Senegal walimiliki mpira zaidi, lakini walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango. Algeria walikuwa makini zaidi, wakilazimisha kipa wa Senegal kufanya saves tano. Ulinzi wa Algeria ulidumu hadi mwisho, wakihifadhi clean sheet.

Baada ya kutamatika kwa mchezo huo, makocha walitoa kauli zao kuhusu mchezo ambapo kocha wa Senegal Mame Moussa Cissé alisema “Tulitoa nafasi nyingi kwa wapinzani. Tumepoteza kwa makosa ya kibinafsi. Tunapaswa kujipanga upya na kuhakikisha tunashinda Kenya.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Algeria walionyesha nidhamu na uthabiti wa mchezo, wakitumia mbinu za mashambulizi na ulinzi kwa usawa. Algeria sasa wako sawa na Morocco kwa pointi tatu, lakini Morocco wanaongoza kwa tofauti ya magoli baada ya ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Kenya. Senegal wako nafasi ya tatu, Kenya wakiburuza mkia.

Mechi zinazofuata zitakua na ukubwa wa kipekee kabisa. Algeria dhidi ya Morocco, hii mechi kubwa inayoweza kuamua hatima ya Kundi A. Vilevile, mchezo wa Senegal dhidi ya Kenya, ni mechi ya lazima kushinda kwa pande zote mbili ili kuendeleza matumaini ya kufuzu.
Kwa Algeria, ushindi huu ni mwanzo bora na ishara ya nia ya kufika mbali kwenye mashindano haya, ambayo pia ni njia ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake 2027 nchini Brazil.


