TAARIFA njema kwa mashabiki na wanachama wa Yanga ni kwamba kiungo wao fundi Khalid Aucho yupo fiti na anaweza akatumika kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC kwenye uwanja wa Mkapa.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Yanga wakiongozwa na Dokta Shecky Mngazija ambao wamesema Aucho ambaye ni raia wa Kimataifa wa Uganda hana shida tena kama ambavyo ilitoke wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

auchoAucho alishindwa kumaliza mchezo huo dhidi ya Mtibwa ambao Yanga walishinda mabao 3-0 uwanja wa Mkapa baada ya kukaa chini kwa maumivu na baadae kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Zawadi Mauya.

Akizungumzia hali ya Aucho Mngazija alisem: “Aucho alipata majeraha ya kawaida tu kwenye mchezo huo mguu ulishtuka tukaona tusiendelee kumuacha uwanjani kwasababu angeweza kupata majeraha makubwa zaidi, ndipo mwalimu akaona ambadilishe kwa ajili ya mapumziko.

“Licha ya kupata jeraha hilo mpaka muda huu tunaozungumza Aucho anaendelea vizuri na analeta matumaini makubwa sana na mashabiki wasiwe na wasiwasi na kiungo huyo kwani anaweza kutumika kwenye mechi ya wikiendi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa