Mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele, ametangaza rasmi kuondoka Pyramids FC baada ya kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya klabu hiyo, akitumia ujumbe wa hisia kuelezea shukrani zake kwa kila aliyeshiriki katika safari yake ndani ya timu hiyo.
Kupitia ujumbe aliouchapisha, Mayele amesema kila hadithi huwa na mwisho, lakini kumbukumbu nzuri hubaki milele. Amemshukuru rais wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzake, mashabiki na kila mtu aliyemwamini tangu siku ya kwanza alipowasili Pyramids FC.
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
Mshambuliaji huyo amesema kipindi chake ndani ya Pyramids FC kimejaa mafanikio, akieleza kuwa waliinua mataji, walipitia nyakati za furaha na kujenga historia ambayo itaendelea kukumbukwa na mashabiki wa klabu hiyo kwa miaka mingi ijayo.
“Kila hadithi ina mwisho, lakini kumbukumbu nzuri hudumu milele. Nashukuru uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu, mashabiki na kila aliyeniamini tangu nilipowasili. Ninaondoka nikiwa na heshima kubwa na shukrani za dhati kwa familia ya Pyramids FC,“ amesema Mayele.
Mayele amesema sasa umefika wakati wa kuanza changamoto mpya katika maisha yake ya soka, huku taarifa zikimtaja kuwa amekamilisha makubaliano ya kujiunga na Ahly Tripoli ya Libya. Hata hivyo, mshambuliaji huyo bado hajaweka wazi rasmi klabu atakayochezea, akiwa kwa sasa mapumzikoni baada ya kumaliza kushiriki michuano ya Dunia


