Barbra Banda Ang'ara kwa Kufunga Mabao Manne, Zambia Yaifumua Sita Misri WAFCON

Nahodha wa Zambia, Barbra Banda, ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye soka la wanawake barani Afrika baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 6-0 dhidi ya Misri katika mchezo wa Kundi C wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 uliochezwa kwenye Uwanja wa Stade Olympique de Rabat nchini Morocco.

Barbra Banda Ang'ara kwa Kufunga Mabao Manne, Zambia Yaifumua Sita Misri WAFCONBanda alikuwa nyota wa mchezo kwa kufunga mabao manne, akianza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 61 kabla ya kuongeza bao la pili dakika ya 64. Aliendelea kung’ara kwa kufunga bao la tatu dakika ya 87 na kukamilisha ‘poker’ yake kwa bao la nne dakika ya 90. Mabao mengine ya Zambia yalifungwa na Racheal Nachula dakika ya 25 na Eneless Phiri dakika ya 90.

mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu

Ushindi huo umeipa Zambia mwanzo mzuri katika kampeni yake ya WAFCON 2026, huku ikipeleka ujumbe mzito kwa wapinzani wake kuhusu dhamira ya kufanya vizuri na kuandika historia nyingine katika mashindano hayo.

Barbra Banda Ang'ara kwa Kufunga Mabao Manne, Zambia Yaifumua Sita Misri WAFCONKwa upande wa Barbra Banda, mabao hayo manne yameendelea kuongeza rekodi yake kama mmoja wa washambuliaji bora zaidi Afrika. Nyota huyo tayari aliweka historia kwenye Michezo ya Olimpiki mwaka 2021 kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa kike kufunga hat-trick mbili mfululizo katika historia ya mashindano hayo.

Barbra Banda Ang'ara kwa Kufunga Mabao Manne, Zambia Yaifumua Sita Misri WAFCON“Mabao manne ya Barbra Banda yamemuingiza kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kufunga mabao mengi katika mchezo mmoja wa WAFCON, akifuata nyayo za gwiji wa Nigeria, Perpetua Nkwocha, aliyefunga mabao manne dhidi ya Cameroon mwaka 2004, pamoja na Asisat Oshoala ambaye alifanya hivyo dhidi ya Mali mwaka 2016.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.