CAF Yatangaza Ratiba Kamili ya Michuano ya Vilabu Afrika 2026/27

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa rasmi ratiba ya mashindano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup msimu wa 2026/27, hatua inayoweka msingi wa msimu mwingine mkubwa wa soka la vilabu barani Afrika. Ratiba hiyo inatoa mwongozo wa muda wote wa mashindano kuanzia hatua za awali hadi fainali.

CAF Yatangaza Ratiba Kamili ya Michuano ya Vilabu Afrika 2026/27

Kwa mujibu wa CAF, hatua za awali (preliminary rounds) zitaanza Septemba 2026, ambapo raundi ya kwanza itachezwa kati ya Septemba 4 hadi 13. Hii itafuatiwa na raundi ya pili ya awali itakayofanyika Oktoba 16 hadi 25, ambapo timu zitapambana kuingia hatua ya makundi.

Hatua ya makundi ya mashindano yote mawili itaanza Novemba 27, 2026 na kuendelea hadi Januari 23, 2027. Mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini utatumika kama kawaida, huku timu bora zikisaka nafasi ya kuingia hatua ya mtoano baada ya mechi sita za kila kikundi.

CAF Yatangaza Ratiba Kamili ya Michuano ya Vilabu Afrika 2026/27

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya hatua ya makundi, robo fainali zitachezwa kati ya Februari 26 hadi Machi 7, 2027, zikifuatiwa na nusu fainali zitakazofanyika Aprili 9 hadi Aprili 17, 2027. Hatua hizi zitakuwa muhimu kuamua timu zitakazofika fainali za mashindano hayo makubwa barani Afrika.

CAF Yatangaza Ratiba Kamili ya Michuano ya Vilabu Afrika 2026/27

CAF pia imethibitisha kuwa fainali za Champions League na Confederation Cup zitafanyika kati ya Mei 9 hadi Mei 31, 2027, ingawa tarehe na maeneo maalum ya fainali hizo bado hayajatangazwa. Ratiba hiyo inatarajiwa kusaidia klabu, mashirikisho ya taifa na wadhamini kupanga vizuri maandalizi ya msimu ujao wa soka la klabu Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.