Infantino Atoa Onyo Kali Baada Ya Fainali Afcon

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amewapongeza Senegal kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco, lakini pongezi hizo zimeambatana na lawama nzito kufuatia matukio mabaya yaliyojitokeza mwishoni mwa fainali hiyo. 

Infantino amesema wazi kuwa vitendo vya vurugu, maandamano na baadhi ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Senegal kuondoka uwanjani havina nafasi katika soka. Ameeleza kuwa ni kosa kubwa kwa timu kuacha uwanja kwa njia hiyo na kusisitiza kuwa heshima kwa waamuzi ni msingi wa mchezo.

Infantino Atoa Onyo Kali Baada Ya Fainali Afcon

Fainali hiyo iligeuka kuwa ya sintofahamu baada ya bao la Senegal kufutwa na baadaye  Morocco kupewa penalti iliyozua mabishano makali. Maamuzi hayo yalichochea hasira kubwa kwa wachezaji wa Senegal, hali iliyosababisha baadhi yao kuondoka uwanjani kwa madai ya kupinga uamuzi wa waamuzi. Mechi ilisimamishwa kwa zaidi ya dakika 16 huku hali ya taharuki ikitawala ndani na nje ya uwanja.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) alijapishana na Infantino, limethibitisha kuanza mchakato wa kuchunguza matukio yote ya fainali hiyo kwa kupitia picha za video, likisisitiza kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kukiuka maadili ya mchezo. CAF imelaani vikali tabia isiyokubalika ya baadhi ya wachezaji na maofisa, ikiahidi kuchukua hatua kali.

Infantino Atoa Onyo Kali Baada Ya Fainali Afcon

Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané, ametoa kauli yake kuhusu tukio hilo na kusisitiza kuwa ingekuwa ni wazimu kwa timu yake kukataa kurejea uwanjani. Mané alihamasisha wachezaji wenzake kurejea kucheza baada ya takribani dakika 16, akisema kuwa kuiacha mechi iishe hivyo kungeliletea soka la Afrika taswira mbaya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.