Juma Mwambusi Ajiunga Ihefu.

Juma Mwambusi kocha wa zamani wa klabu ya Mbeya City,Azam, na Yanga amefanikiwa kujiunga na klabu ya Ihefu Fc ya jijini Mbeya.

Kocha huyo ametangazwa leo rasmi na mabingwa hao wa ligi daraja la kwanza na kupanda ligi kuu baada kushuka misimu kadhaa nyuma imefanikiwa kupanda tena na kushiriki ligi ya msimu wa 2022/23.

juma mwambusiIhefu ilifanikiwa kua mabingwa wa ligi daraja la kwanza chini ya mwalimu Zuberi Katwila ambae ndie alikua kocha mkuu wa timu hiyo mpaka Juma anatangazwa kua kocha mkuu jambo ambalo limeacha sintonfahamu kwani hakuna taarifa ya timu hiyo kutoa ufafanuzi juu ya kuachana na mwalimu Katwila na zaidi wameeleza kocha huyo atakuja kuungana na benchi la ufundi la trimu hiyo.

Ihefu ambao hawajashinda mchezo wowote wa ligi kuu Tanzania bara mpaka sasa ambapo tayari imeshachezwa michezo minne kitu ambacho kinatafsiriwa kusababisha timu hiyo kumleta mwalimu Juma Mwambusi.

Acha ujumbe