Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Veron Mosengo-Omba, ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake, akihitimisha safari yake ya zaidi ya miongo mitatu katika utumishi wa soka barani Afrika.
Mosengo-Omba amesema uamuzi wake umetokana na hitaji la kupumzika na kuelekeza nguvu zake kwenye maisha binafsi baada ya miaka mingi ya kazi. “Ninaondoka kwa amani kabisa, nikiwa na furaha ya mchango nilioutoa katika maendeleo ya soka la Afrika,” alinukuliwa akisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hatua hiyo ya kujiuzulu imekuja katika kipindi ambacho CAF inakabiliwa na mjadala mpana kuhusu maandalizi na usimamizi wa michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika nchini Morocco.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, kipindi cha hivi karibuni cha uongozi wake kimekuwa na changamoto kadhaa za kiutawala, huku kukiwa na mvutano juu ya mwelekeo wa maendeleo ya soka barani Afrika. “Kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa wadau kuhusu uwazi na usimamizi wa michuano mikubwa,” amesema mmoja wa wachambuzi wa michezo.
Licha ya changamoto hizo, Mosengo-Omba anaondoka akiwa ameacha alama katika utawala wa soka Afrika, hasa katika kusimamia programu mbalimbali za maendeleo. “Ni safari ndefu yenye mafanikio na mafunzo mengi, na nina imani soka la Afrika litaendelea kukua,” aliongeza.
Kujiuzulu kwake kunatarajiwa kufungua ukurasa mpya ndani ya CAF, huku wadau wakisubiri kuona nani atakayechukua nafasi hiyo muhimu katika kipindi hiki nyeti kuelekea michuano mikubwa ijayo.

