Kenya Hatarini Kupoteza Haki ya Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027

Kenya inakabiliwa na hatari ya kupoteza nafasi yake ya kuwa mwenyeji mwenza wa AFCON 2027 kutokana na ucheleweshaji wa kulipa ada ya uenyeji ya Shilingi bilioni 3.9 (sawa na dola milioni 30) kwa CAF.

Kenya Hatarini Kupoteza Haki ya Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Elijah Mwangi, alibainisha Alhamisi kuwa malipo hayo lazima yakamilishwe ifikapo Machi 30, 2026, kama sehemu ya zabuni ya pamoja ya “East Africa Pamoja” inayohusisha Uganda na Tanzania.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Michezo na Utamaduni inayoongozwa na Dan Wanyama, Mwangi alisema Uganda na Tanzania tayari zimekamilisha malipo yao, huku Kenya ikiwa bado haijatimiza wajibu huo. Alionya kuwa ucheleweshaji huo unaweza kudhoofisha uaminifu wa Kenya kama mwenyeji wa mashindano hayo.

Mwangi alisisitiza kuwa CAF imetoa muda hadi Machi 30 kukamilisha malipo hayo, na kushindwa kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha maandalizi yote yaliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya AFCON 2027. Aidha, aliweka wazi kuwa viwanja vya Kasarani Stadium na Nyayo Stadium huenda visikamilike kwa wakati kulingana na muda uliowekwa na CAF.

Kenya Hatarini Kupoteza Haki ya Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027Aidha, aliweka wazi kuwa mkandarasi wa ukarabati wa Kasarani amepunguza wafanyakazi kutokana na deni la Shilingi bilioni 3.7, huku mkandarasi wa Nyayo akiondoka kabisa kutokana na deni la Shilingi bilioni 2.7, hali inayoongeza changamoto kwa maandalizi ya michuano hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.