Malawi Yaishangaza Afrika kwa Kuivunja Rekodi ya Nigeria WAFCON

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON), Nigeria, wameanza vibaya safari yao ya kutetea taji baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-2 kutoka Malawi katika mchezo wa Kundi C uliopigwa kwenye Uwanja wa Stade El Barid nchini Morocco.

Malawi Yaishangaza Afrika kwa Kuivunja Rekodi ya Nigeria WAFCONBaada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare tasa, Malawi ilianza kuonyesha makali yake kipindi cha pili ambapo Temwa Chawinga aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 73. Dada yake, Tabitha Chawinga, aliendeleza shinikizo kwa kufunga bao la pili dakika ya 79 na kuiweka Malawi kwenye nafasi nzuri ya ushindi.

mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu

Nigeria ilijaribu kurejea mchezoni kupitia penalti iliyofungwa na Rasheedat Ajibade dakika ya 90+2, lakini Temwa Chawinga aliizamisha tena kwa kufunga bao la tatu dakika ya 90+5. Uchenna Kanua aliifungia Nigeria bao la pili katika dakika za nyongeza, lakini halikutosha kuzuia kipigo hicho.

Malawi Yaishangaza Afrika kwa Kuivunja Rekodi ya Nigeria WAFCONUshindi huo umeifanya Malawi kuandika historia kwa kuifunga Nigeria kwa mara ya kwanza kabisa katika hatua ya fainali za WAFCON. Aidha, kasi na ubora wa Temwa pamoja na Tabitha Chawinga uliwapa wakati mgumu mabeki wa Nigeria katika mchezo mzima.

Malawi Yaishangaza Afrika kwa Kuivunja Rekodi ya Nigeria WAFCON“Kwa Nigeria, hiki ni kipigo cha tatu mfululizo katika mchezo wa ufunguzi wa WAFCON baada ya pia kupoteza dhidi ya Afrika Kusini mwaka 2018 na 2022. Sasa Super Falcons watalazimika kushinda mchezo wao ujao dhidi ya Zambia utakaochezwa Agosti 1 ili kujiweka kwenye nafasi nzuri y  a kutinga hatua ya robo fainali, huku Zambia ikiingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali kubwa baada ya kuifunga Misri mabao 6-0.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.