Staa wa zamani wa klabu ya Yanga Saidoo Ntibazonkiza inaelezwa amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Geita Gold  mkoani Shinyanga.
Ntibanzonkiza ambae aliachana na klabu yake ya zamani baada ya mkataba wake kumalizika na waajiri wake hao licha ya kua na matatizo ya kinidhamu na klabu yake hiyo ya zamani.
Ntibanzonkiza
Ntibanzonkiza

Geita wanamsajili Saidoo kwajili ya kuongeza nguvu katika klabu hiyo ambayo inakwenda kushiriki michuano ya shirikisho ya afrika.

Nyota huyo alievitumikia vilabu kadhaa barani ulaya ameamua kujiunga na matajiri hao Shinyanga baada kutoka mapumziko kidogo kutoka kwao Burundi.

Ligi ya Tnzania inaoenekana kukua kwa kasi sana kwani vilabu vinaweza kuwapata wachezaji wenye wasifu mkubwa kuweza kuvitumikia vilabu hivo hali hii iliozoeleka kwa vilabu vikubwa hasa Simba,Yanga, na Azam.

Lakini kwa wakati huu hata vilabu vya kawaida vinaweza kuwapata wachezaji wakubwa kutoka nje ya nchi hii inaonesha namna ligi ya ndani imekua kwa kiwango kikubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa