Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, Michael Olunga, ameondolewa katika kikosi cha mwisho kitakachoshiriki michuano ya FIFA Series 2026 itakayofanyika mjini Kigali kuanzia Machi 27.
Kocha mkuu Benni McCarthy ametangaza kikosi cha wachezaji 23 akibainisha kuwa mabadiliko hayo yametokana na majeraha pamoja na kutokuwepo kwa baadhi ya nyota waliokuwa kwenye kikosi cha awali. Kwa mujibu wa shirikisho la soka la kenya, marekebisho hayo yalikuwa muhimu ili kupata kikosi kitakachosafiri kwa ajili ya mashindano hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mbali na Olunga, wachezaji wengine walioachwa ni pamoja na Byrne Omondi, Erick Ouma, Joseph Okumu, Sylvester Owino, Collins Sichenje, Tyler Onyango, Andre Gitau, Adam Wilson na Jonah Ayunga, huku Daniel Anyembe na Zak Vyner wakithibitishwa kutokuwepo kutokana na sababu mbalimbali.
Kupitia taarifa ya FKF, ilielezwa “Baadhi ya wachezaji hawapatikani kwa dirisha hili la kimataifa kutokana na majeraha na sababu nyinginezo, hivyo benchi la ufundi limeamua kufanya mabadiliko kwenye kikosi kitakachosafiri.”
Kenya itaanza kampeni yake kwa kucheza dhidi ya Estonia katika dimba la Amahoro Stadium, huku mchezo wa pili ukitegemea matokeo ya pambano kati ya Rwanda na timu ya taifa ya Grenada.
Mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya Kenya kuelekea AFCON 2027, ambayo yataandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania, huku yakitoa fursa kwa timu hiyo kujipima dhidi ya mataifa kutoka mabara tofauti.


