BAADA ya kuanza michuano ya Championship kwa sare ugenini dhidi ya Kitayosce, benchi la ufundi la Pan African limefurahishwa na viwango vya wachezaji wao na kuahidi kufanya vizuri msimu huu.

Mchezo huo wa kwanza kwa timu zote ulipigwa jana jumamosi kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Pan African, Twaha Beimbaya amesema kuwa “Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kumaliza salama mchezo wetu na kupata pointi moja ugenini.

“Mchezo ulikuwa mgumu na kwa upande wangu nimepata uzoefu wa mechi hizi za ugenini hivyo tunaenda kupambana kwenye mchezo ujao wa ugenini dhidi ya Mashujaa.

“Tunaahidi kufanya vizuri kwenye michuano ya Championship kwa msimu huu na kuipeleka Pan sehemu ambayo ni sahihi kwa maana ya kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa