Gwiji wa soka wa Patrice Evra mwenye asili ya Senegal amemwaga povu kufuatia uamuzi wa CAF wa kuivua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuipatia Morocco. Evra amedai kuwa kitendo hicho ni “kujishusha thamani” kwa soka la Afrika na kuongeza kuwa dunia inaitazama Afrika kwa kicheko.
“Nilivyoiona taarifa ya Morocco kuwa mabingwa, nilijua ni siku ya wajinga (April Fool’s),” alisema Evra, huku akisisitiza kuwa bingwa wa kweli uwanjani ni Senegal.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Uamuzi wa CAF unakuja baada ya kubatilisha matokeo ya fainali ya Januari 18, 2026, ambapo Senegal iliondoka uwanjani kulalamikia penalti ya dakika za lala salama. Kwa mujibu wa ripoti za ESPN na vyanzo vingine, Morocco sasa wametangazwa washindi wa 3-0 kwa kanuni za Forfeit, ambazo zinatumika pale timu inashindwa kufika au kukataa kuendelea na mchezo.
Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) tayari limetangaza kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), wakidai kuwa timu yao imeonewa haki. Uamuzi huu umeibua mjadala mkali barani Afrika na duniani kote, huku mashabiki na wachezaji wakijadili iwapo Morocco wana ubingwa halali au Senegal wameonewa katika matokeo haya.

