Baada ya kuandika historia ya dhahabu kwenye ardhi ya Afrika, mashujaa wa Senegal wamepokea heshima inayolingana na ukubwa wa mafanikio yao. Rais wa nchi hiyo, Bassirou Diomaye Faye, ametangaza zawadi nono kwa wachezaji wa timu ya taifa kama pongezi kwa kazi kubwa waliyoifanya.
Kila mchezaji wa kikosi cha Taifa cha Senegal atapokea Euro 115,000 taslimu, sawa na takribani Shilingi milioni 339, sambamba na kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1,500 katika mji mkuu Dakar. Ni ishara ya kuthamini jasho lililomwagika uwanjani na mchango wa kila nyota aliyepigana kwa nembo ya taifa.
Sio wachezaji pekee walioguswa na mkono wa shukrani wa serikali. Viongozi na wajumbe wa Shirikisho la Soka Senegal pia wameingizwa kwenye orodha ya wanaonufaika, kila mmoja akipokea Euro 75,000 (takribani Shilingi milioni 217) pamoja na kiwanja cha kujenga makazi, kuthibitisha kuwa mafanikio ya soka ni matokeo ya kazi ya timu nzima ndani na nje ya uwanja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa serikali, wale wote kutoka Wizara ya Michezo waliokuwa sehemu ya msafara wa timu ya taifa hawakusahaulika. Kiasi cha Euro 465,000, sawa na takribani Shilingi bilioni 1.36, kimetengwa kugawiwa kwa pamoja kama motisha na pongezi kwa mchango wao katika safari ya ushindi.
Zawadi hizi zimekuja baada ya Senegal kutwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kishindo, wakiwazamisha wenyeji Morocco kwa bao 1-0 kwenye fainali. Ushindi huo umeifanya Senegal sio tu mabingwa wa Afrika, bali taifa linalothibitisha kuwa ushindi wa soka ni uwekezaji wa fahari na heshima ya kudumu.