Serengeti Boys Yapangwa Kundi C AFCON U-17 Morocco 2026

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, imepangwa katika Kundi C la michuano ya AFCON U-17 2026 itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Mei 13 hadi Juni 2, 2026. Katika kundi hilo, Serengeti Boys watakutana na timu za Mali, Angola na Msumbiji.

Serengeti Boys Yapangwa Kundi C AFCON U-17 Morocco 2026Droo ya upangaji wa makundi hayo imefanyika leo kwa kusimamiwa na mastaa mbalimbali wa soka barani Afrika, akiwemo Fiston Mayele wa Pyramids FC, Aliou Dieng wa Al Ahly SC pamoja na Ahmed Belhadj wa Ceramica Cleopatra FC.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kundi la Serengeti Boys linatajwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa Mali, ambao ni moja ya mataifa yenye historia nzuri katika soka la vijana barani Afrika. Hata hivyo, Angola na Mozambique pia zinatarajiwa kutoa upinzani mkali katika mbio za kusaka tiketi ya hatua inayofuata.

Serengeti Boys Yapangwa Kundi C AFCON U-17 Morocco 2026Makundi mengine yamejumuisha wenyeji Morocco, Tunisia, Misri na Ethiopia katika Kundi A, huku Kundi B likiwa na Côte d’Ivoire, Cameroon, Uganda na DR Congo. Kundi D linaundwa na Senegal, Afrika Kusini, Algeria na Ghana, zote zikiwa timu zenye ushindani mkubwa.

Serengeti Boys Yapangwa Kundi C AFCON U-17 Morocco 2026Serengeti Boys wanatarajiwa kuingia kwenye michuano hiyo wakiwa na lengo la kufanya vizuri na kuipeperusha bendera ya Tanzania, huku matarajio ya wengi ni kuona kizazi kipya cha vipaji kikionyesha uwezo mkubwa katika soka la Afrika kama ilivyowahi kutokea 2017.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.