Klabu ya soka ya Simba inaelezwa ipo mbioni kumalizana na kocha wa klabu ya Vipers mbingwa wa soka nchini Uganda Robertinho Oliviera.

Kocha huyo ambaye amekua na msimu bora na klabu hiyo ya nchini Uganda na inaelezwa amewavutia mabosi wa klabu ya Simba miamba hiyo ya soka nchini Tanzania.

simbaSimba kwasasa hawajapata kocha mkuu baada ya kuondokewa na kocha wao mkuu Zoran Maki alietimkia klabu ya Al-Itihhad ya nchini Misri hivo klabu hiyo haijapata kocha mkuu huku wakiwa na kaimu kocha mkuu ambaye anaiongoza timu hiyo kwasasa Juma Mgunda pamoja na msaidizi wake Selemani Matola.

Kocha huyo raia wa Brazil inasemakana amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye klabu hiyo ya Vipers na Simba wapo tayari kununua mkataba huo ili wampate mwalimu huyo aweze kutua katika timu hiyo.

Mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili hivo wakikubaliana basi inawezekana kocha huyo akaonekana katika viunga vya Bunju akifundisha timu hiyo.