Klabu ya soka ya Simba kupitia msemaji wake bwana Ahmed Ally ameeleza kikosi hicho kitasafiri kesho siku ya Ijumaa kuelekea Visiwani Zanzibar.

Katika safari hiyo ya kuelekea Visiwani Zanzibar inaelezwa timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kujipima nguvu katika kipindi hichi.

Wakati huu ambao kuna mapumziko kwajili ya kupisha mechi za kimataifa ambapo kikosi kitakachosafiri kuelekea Visiwani Zanzibar ni wale wachezaji pekee ambao hawajapata nafasi ya kuitwa kwenye timu zao za taifa.

simbaSimba imekua na utaratibu wa kupata mechi za kirafiki wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa kitu kinachowasaidia kuleta utimamu wa kimwili kwa wachezaji wao katika wakati huu wanapojiandaa kuelekea michuano ya kimataifa mapema mwezi wa kumi.


Ikumbukwe baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa klabu hiyo inakwenda kukumbana na kibarua cha mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Premire de Agosto kutoka nchini Angola hivo ni muhimu kwa klabu hiyo kucheza mechi za kirafiki ili kujenga utimamu wa kimwili wa wachezaji wao kuelekea mchezo huo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa