Klabu ya soka ya Simba imepanga kutumia mapumziko ya mechi za kimataifa kujipima nguvu na vilabu kadhaa vikubwa vya nje ya Tanzania.

Klabu ya Simba itacheza michezo hiyo dhidi ya Al Hilal ya Sudani, Asante Kotoko ya nchini Ghana, pamoja na AS Arta Solar ya nchini Djibouti. Mechi hizo zitachezwa mbili nje ya Tanzania kwa maana ya Sudani ambapo kuna michuano maalumu ambayo imeandaliwa na klabu ya Al Hilal ya nchini humo.

simba, Simba Kujipima Kikubwa., Meridianbetsimba simba

Ambapo Simba watacheza mchezo wao wa kwanza na Asante Kotoko Agosti 28, na mechi ya pili itachezwa Agosti 31 huku mchezo wa mwisho ukipigwa Septemba tatu jijini Dar-es-salaam dhidi ya As Arta Solar team ambayo amewahi kucheza mchezaji wa zamani wa vilabu vya Arsenal pamoja Fc Barcelona.

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez ameeleza “kualikwa na Al Hilal kwenye michuano hii maalumu ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wetu na klabu mbalimbali barani Afrika,Haaya ni matumda ya mahusiano yaliyojengwa kwenye michuano ya Simba super cup 2021.

“Ikumbukwe mwaka 2021 Simba iliandaa michuano yake ikifahamika kama Simba super cup ikishirikisha timu kama Al Hilal ya Sudani pamoja Tp Mazembe ya nchini Congo. Hivo uhusiano anaoungelela mtendaji mkuu wa klabu ulianza kujengwa huku mpaka leo hii Simba nae anaalikwa na Al Hilal ya sudani kwenye michuano maalumu iliandaliwa na klabu hiyo nchini humo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa