Klabu ya soka ya wanawake ya Simba Simba Queens imetangaza iko tayari kwa michuano ya ligi ya mabingwa Afrika wakiwa kama wawakilishi pekee wa ukanda wa Cecafa kwenye michuano hiyo.simba queensAkizungumza na wanahabari Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amezungumza na kusema timu hiyo ya wanqawake ipo tayari kwa michuano hiyo kwani itasafiri kesho alfajiri kuelekea nchini Morocco ambapo michuano hiyo itakapofanyika hivo timu hiyo ikijumuisha wachezaji 25 itasafiri kesho alfajiri oktoba 26.

Simba Queens imefanikiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kubeba ubingwa wa cecafa inayohusisha timu kutoka Afrika mashariki hivo kuwapatia nafasi klabu hiyo kupata uwakilishi pekee kutoka Afrika mashariki katika ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hiyo ya wanawake ya Simba imekua ikifanya vizuri kwa miaka kadhaa sasa kwani ligi ya nyumbani tayari wameshabeba ubingwa ligi ya wanawake mara tatu mfululizo.simba queensHuku kocha mkuu wa Simba Queens akisema hakuna majeruhi hata mmoja kwenye kikosi hicho akisema vijana wake wapo hali ya utimamu na ushindani kwani wamecheza mechi kadhaa za kirafiki hivo kikosi chake kipo tayari kupambana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa