Klabu ya Simba imerejea jijini Dar es salaam ikitokea Uganda baada ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Vipers kwa kumtandika bao 1-0 akiwa nyumbani kwake kwenye uwanja wa St Marrys.

 

Bao hilo lilifungwa na beki wa kati wa Simba Henock Inonga katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya mnyama kusaka sana bao kwenye lango la Vipers ambayo bado haijapata ushindi.


Roberto na vijana wake wamerejea nchini huku wakijiandaa kwaajili ya mchezo ujao wa marudiano na Vipers huku wakihitaji ushindi pekee ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye michuano hii.

Mechi hiyo itapigwa tarehe 7 mwezi Machi katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 11:00 jioni wakati huo huo mnyama atakuwa akiomba Horoya apoteze ili yeye ashikilie nafasi ya pili.

Hivyo basi kocha ana kazi nzito ya kufanya kwaajili ya kuhakikisha anapata ushindi pekee Benjamin Mkapa siku hiyo ya Jumanne.

 

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa