Klabu ya Simba imefanikiwa kupata alama tatu dhidi ya klabu ya Prisons ya mkoani Mbeya kwa ushindi wa bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Sokoine.

Mchezo huo ambao ulionekana kuchukuliwa na klabu ya Simba kuanzia kipindi cha kwanza mpaka kipindi cha pili cha mchezo wekundu hao wa msimbazi walikua bado wameushikilia mchezo wakitafuta namna ya kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo.

simbaKwenye mchezo huu Simba walihitaji alama tatu muhimu ili kuendelea kukaa kwenye nafasi nzuri kwani watani wao walishapata matokeo mazuri katika mchezo wao wa jana dhidi ya walima miwa wa mkoani morogoro klabu ya Mtibwa Sugar.

Simba chini ya Mwalimu Juma Mgunda ambae anaiongoza timu hiyo kwenye mechi ya pili ya kimashindano imefanikiwa kupata alama tatu mkoani Mbeya ambapo mara ya mwisho kucheza mkoani hapo walipoteza kwa bao moja kwa bila.

Ni Jonas Mkude ambae aliwainua mashabiki wa mnyama dakika ya 86 baada ya pasi safi kutoka kwa Kibu Denis na kuipa timu hiyo alama tatu na kuwafanya kufuta uteja katika uwanja wa Sokoine ambao umekua mgumu kwao kwa muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa