Twiga Stars Yatupwa Nje Wafcon 2026 Baada ya Kupigwa na Ivory coast

Twiga Stars imeondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ivory Coast katika mchezo wa mwisho wa Kundi B uliochezwa jijini Casablanca, Morocco.

Twiga Stars Yatupwa Nje Wafcon 2026 Baada ya Kupigwa na Ivory coastIvory Coast ilianza kuonyesha ubora wake kipindi cha kwanza ambapo Nsira Ouedraogo aliifungia timu hiyo bao la kuongoza dakika ya 44, kabla ya Iines Konan kuongeza bao la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 68 na kuiweka timu yake katika nafasi nzuri ya kupata ushindi.

mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu

Twiga Stars ilipata nafasi ya kupunguza tofauti ya mabao baada ya kupewa penalti dakika ya tisa ya muda wa nyongeza, ambapo Diana Msewa alifanikiwa kufunga na kuleta matumaini mapya kwa Tanzania, lakini muda haukutosha kuibadili hali ya mchezo.

Twiga Stars Yatupwa Nje Wafcon 2026 Baada ya Kupigwa na Ivory coastMatokeo hayo yameifanya Ivory Coast kumaliza kileleni mwa Kundi B ikiwa na pointi saba na kufuzu hatua ya robo fainali, huku Afrika Kusini ikimaliza nafasi ya pili baada ya kuifunga Burkina Faso bao 1-0. Twiga Stars imehitimisha hatua ya makundi ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi tatu.

Licha ya kuondolewa kwenye mashindano hayo, Twiga Stars imeandika historia kwa kupata ushindi wake wa kwanza katika fainali za WAFCON na kufanikiwa kufunga angalau bao moja katika kila mchezo wa hatua ya makundi, jambo linaloonyesha hatua ya maendeleo ya soka la wanawake nchini Tanzania.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.