Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga kupitia rais wake Mhabdishi Hersi Said, amesema wataanza kutangaza vijana watakaoitumikia klabu hiyo kwenye idara ya mawasiliano.

Katika ghafla ya kutangaza mkurugenzi mkuu mtendaji wa klabu hiyo mapema leo,Ndipo Rais wa klabu ya Yanga akagusia kuhusu suala hilo kwakua ni suala linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi,mashabiki,na wafatiliaji wa klabu hiyo.

yangaJioni ya leo itakua ni siku rasmi ya kuanza kuwatangaza watu watakaokua wanahusika na kitengo cha mawasiliano cha klabu, ambapo mpaka sasa hawajakua na afisa habari rasmi wa klabu.

Baada ya kutangaza vijana hao tukio kubwa linalosubiriwa kwa ukubwa ni utambulisho wa afisa habari mpya ambaye atakwenda kuchukua nafasi ya Hassan Bumbuli ndani ya timu hiyo.

Kama ambavyo inaelezwa Ali kamwe kutoka Azam Media ndo anakwenda kua afisa habari mpya na mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha klabu hiyo ya wananchi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa