Klabu ya Yanga imetambulisha Mkurugenzi mtendaji mpya anayejulikana kama Andre Mtine klabuni hapo mapema leo, kupitia Rais wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said Ally.

 

Rais Hersi

Hii imekuja baada ya kuondoka kwa aliyekuwa mkurugenzi mtendaji mkuu wa klabu hiyo raia wa Afrika Kusini Senzo Mbatha, ambaye aliitumikia klabu hiyo ya wananchi kwa takribani miaka miwili baada ya kutoka klabu ya Simba, kabla ya miezi kadhaa nyuma klabu hiyo kutangaza kuachana mkurugenzi huyo.

yangaAndre Mtine ambaye ndio mkurugenzi mpya wa klabu ya Yanga, akipewa mkataba wa miaka miwili ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika ambapo amepita klabu tofauti tofauti barani Afrika, kama Bidco Zesco,amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka nchini Zambia,amefanikiwa kufanya kazi na shirikisho la soka barani Afrika kama mjumbe wa kamati ya fedha, huku funga kazi ikiwa kuitumikia klabu kongwe na yenye mafanikio barani Afrika Tp Mazembe ya nchini Congo.

Pia katika shughuli hiyo Rais wa klabu ametumia fursa hiyo kutambulisha tovuti mpya ya klabu hiyo ambayo itarahisisha mashabiki,wanachama,na wapenzi wa Yanga kupata taarifa ,na maudhui mbalimbali kuhusiana na timu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa