Baada ya maafisa wa Man United kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Eduardo Camavinga, ni dhahiri mchezaji huyo anataka kucheza Uhispania na sio EPL.

Maongezi yaliyofanyika kati ya pande mbili zinazohusika kwenye mchakato huu, yameonekana kutokuwa na ishara chanya kwa United ambao hawapotayari kusajili mchezaji ambaye akili na malengo yake hayapo kwenye klabu yao.

Camavinga amekuwa kwenye rada za United kwa miaka 3 na kwa hali ilivyo, klabu yake (Rennes) inataka kumuuza majira haya kwani atakuwa mchezaji huru muda kama huu mwakani [asiposaini mkataba mpya na klabu hiyo].

Camavinga, Camavinga Anataka Kucheza Kwenye LaLiga., Meridianbet

Camavinga (miaka 18) amekuwa kwenye kiwango bora ukilinganisha na umri wake na anahusishwa na Real Madrid pamoja na Bayern Munich. Japokuwa, ni uhalisia kuwa vilabu vingi duniani kote vimeathiriwa na COVID19 na hivyo kwa Madrid, kama ilivyo kwa mahasimu wao – Barcelona, wanasajili wachezaji huru ikiwa ni sambamba na kujaribu kuuza baadhi ya wachezaji ili kuweka sawa uchumi wa vilabu vyao.

Man United wanahitaji kusajili mchezaji hodari katika safu ya kiungo ukizingatia hali ya sintofahamu kuhusu Paul Pogba ambaye anaingia kwenye mwaka wake 1 wa mwisho klabuni hapo. Mpaka sasa, Pogba amegoma kusaini mkataba mpya na United na kuna kila ishara kuwa mchezaji huyo ataondoka United majira haya au kama mchezaji huru msimu ujao.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa