Dani Carvajal ana sumbuliwa na jeraha jingine na anajiandaa kuikosa michezo mitatu na mlinzi huyo wa Real Madrid ameripotiwa kuwa nje ya dimba kwa mpaka mwisho wa msimu.
Carvajal Nje ya Dimba Mpaka Mwisho wa Msimu
Mlinzi wa Real Madrid Dani Carvajal

Carvajal alikuwa nje kwa miezi miwili mapema mwaka huu kutokana na tatizo la harmstring lakini alirejea dimbani Aprili 21, akitokea benchi katika ushidni wa 3-0 dhidi ya Cadiz.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alicheza dakika 68 katika sare ya 0-0 dhidi ya Real Betis wikendi iliyopita wakati pia alikuwa mchezoni katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea kwenye michuano ya Champions League siku ya Jumanne.

Lakini Real Madrid ilitangaza siku ya Jumanne kwamba amepata majeraha kwenye misuli katika paja lake la kulia ingawa hawakuweka wazi ni lini atarejea.

“Kufuatia vipimo vilivyofanywa leo kwa mchezaji wetu Dani Carvajal na idara ya matibabu ya Real Madrid, amekutwa na tatizo la majeraha ya misuli katika mguu wake wa kulia, ataendelea kupata matibabu,” hiyo ilikuwa taarifa fupi kutoka kwenye klabu hiyo ya LaLiga.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa