Nyota wa PSG ambaye ni kiongozi wa magoli wa wakati wote kule Ligue 1, Edinson Cavani  baada ya  kujiunga na klabu hiyo akitokea Napoli mwaka 2003 anatarajia kustaafu soka, kwa sasa anasema anafikiria kufanya uamuzi huo.

Nyota huyu ambaye anatarajia kufikisha umri wa miaka 32 mapema mwezi Februari alianza kucheza soka lake la kulipwa akiwa na Montevideo -Danubio. Mkataba wake na klabu ya PSG unaisha mwisho wa msimu ujao, yeye ameongelea uwezekano wa kutundika daluga baada ya miezi 18 kuanzia sasa.

Cavani anaamini mambo yanaweza kubadilika kuhusu ushiriki wake katika soka, japokuwa hana uhakika nini kitatokea baada ya 2020 lakini kwa sasa anataka kwanza kuumaliza mkataba wake na klabu ya PSG. Hata hivyo, anatarajia kuwa baada ya kumaliza mkataba wake na kurejea Uruguay basi hatakuwa akichezea tena soka Nchi hiyo kwa sababu anahitaji kupumzika na familia yake.

Fundi huyu amechapa Hat-trick kwenye ushindi wa PSG wa bao 9 dhidi ya Guingap jana Jumamosi. Hata hivyo ana wasiwasi chochote kinaweza kutokea katika madirisha ya uhamisho akisema maamuzi wakati wote huwa hayategemei mchezaji. Yanaweza kufanyika maamuzi yeyeote na akajikuta ana staafu akiwa klabu nyingine sio PSG tena.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa