Cavani anasema mazingira mazuri yana kila mchango kwenye kumtengeneza mchezaji kujiona bora na kuonesha kiwango kizuri awapo uwanjani. Zikiwa zimepita siku kadhaa tu tangu mshambuliaji huyo aongeze mkataba, Edinson ameamua kufunguka sababu zilizomfanya asalie United.

Katika mazungumzo na kipindi maalum cha Man United TV, Edinson alieleza kuwa kwa kiwango kikubwa wachezaji wenzake wamechangia yeye kusalia klabuni hapo. Cavani ameonesha furaha yake kwa viongozi, staff, wachezaji, mashabiki na kila mdau wa Manchester United kwa kumuamini.

Cavani aliongeza kuwa kuna wakati wachezaji wenzake walimwambia asiondoke bado wanamuhitaji na wanatamani aendelee kusalia hapo. Na bila hiyana yeye akaamua kusalia hapo ili kuendelea kufurahia maisha pale United.

Vilevile imani kubwa aliyoonesha kocha wake Ole imemuongezea kujiamini kukubwa na kuamini kuwa anaweza kuwa na wakati mzuri pale OT, mpaka sasa Edinson amekuwa na wakati mzuri sana pale United toka arudi kutoka Ufaransa.

Cavani ameongeza mkataba wa mwaka mmoja lakini kuna baadhi ya watu wanaonekana kutoridhishwa na suala hilo kwa kudai kuwa United inahitaji vijana kwa sasa.

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

cavani, Cavani: Wachezaji Wenzangu Wamechangia Sana Mimi Kusalia OT, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa