Mkurugenzi wa Inter Milan Beppe Marotta amesisitiza kwamba Romelu Lukaku hauzwi hali yakuwa kumekuwa na uvumi mkubwa kuhusu hatima ya mshambuliaji huyo wa Belgium.

CEO Marotta Asisitiza Kuwa 'Lukaku Hauzwi'

Lukaku amekuwa akihusishwa kuondoka lutoka kwa mabingwa hao wa Italia kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Antonio Conte na The Nerazzurri wamekuwa wakipambana na hali ya kiuchumi iliyosababishwa na ugonjwa wa corona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameripotiwa kuvuta hisia za klabu yake ya zamani ya Chelsea na mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City.

Akizungumza kabla ya mchezo wa kirafiki wa Inter na Wapergoleti, Marotta alikomesha mazungumzo juu ya Lukaku kuondoka San Siro.

“Kutoka upande wetu, tunaweza kusema kwamba, Lukaku hauzwi,” Marotta aliiambia Sportmediaset. “Lukaku ni kipande muhimu kwenye timu inayopatikana kwa kocha mkuu Simone Inzaghi.”

Lukaku alifunga mabao 24 katika michezo 36 ya ligi msimu 2020-21, wakati pia alitoa assist 11.

Ni msimu wa 2016-17 tu alipokuwa Everton ambapo Ubelgiji huyo alifunga zaidi 25 katika kampeni moja katika moja ya ligi tano bora za Ulaya.

Lukaku anatarajiwa kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza chini ya Inzaghi siku ya Jumatatu.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa