Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Clatous Chama amefunguka kuwa kikosi chao sasa kinajipanga kuhakikisha wanavuka hatua hiyo na kucheza nusu fainali.

Chama

Licha ya kusaliwa na mechi moja mkononi, Simba Jumamosi iliyopita ilifanikiwa kujihakikishia nafasi ya kumaliza kinara wa msimamo wa kundi A baada ya kuifunga AS Vita na kufikisha pointi 13.

Kwenye ushindi huo wa mabao 4-1 walioupata juzi dhidi ya AS Vita, Chama alihusika katika mabao matatu, akifunga mabao mawili na kusaidia bao moja lililofungwa na Rally Bwalya.

Chama

Akizungumzia malengo yao Chama amesema: “Kama timu tuna furaha kubwa kwa kuweza kupata nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, lakini si tu kwamba tumeingia hatua ya robo fainali, bali tumefanikiwa kumaliza kama vinara wa kundi letu.

“Tunajua ushindi wa vita hii ni mwanzo wa vita nyingine ya kuitafuta nusu fainali, tunajua haitakuwa rahisi lakini tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michezo yetu ya robo fainali na tutajitoa kwa kila kitu ili kufuzu nusu fainali na kufika mbali zaidi,”


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

chama, Chama: Tutafika Nusu Fainali CAFCL, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa