Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea siku ya Jumanne kwa mchezo wa Bingwa mtetezi Chelsea wakiwaalika Lille kutoka Ligue 1 katika dimba la Stamford Bridge ikiwa ni hatua ya raundi ya 16 bora.

Chelsea Watanguliza Mguu Mmoja Robo Fainali

Chelsea ilianza mchezo wakiwa na nguvu na kutengeneza nafasi tatu na kufanikiwa kupata bao dakika ya 8 kupitia kwa mchezaji Kai Havertz baada ya kujaribu mara mbili na kukosa.

Mabigwa watetezi wa Ligue 1 walishindwa kabisa kufurukuta mbele ya vijana wa Tuchel licha ya kuwa na wachezaji machachari kama Renato Sanches na wamekuwa na wakati mgumu sana msimu huu hata kwenye ligi kuu ya Ufaransa wakikaa nafasi ya 11 kwenye msimamo.

Chelsea walipata bao la pili kupitia kwa Christian Pulisic baada ya kupata pasi safi kutoka kwa N’Golo Kante dakika ya 63 ya mchezo.

Mchezo wa marudiano utapigwa mwei Machi 16 katika dimba la Stade Pierre-Mauroy Ufaransa Lille watahitaji ushindi wa magoli zaidi ya mawili ilikusonga hatua ya robo fainali.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa