Joshua Kimmich ameongeza kandarasi yake na Bayern Munich hadi 2025 siku ya Jumatatu, kulingana na tovuti rasmi ya klabu.
Akiwa na uwezo wa kucheza kwenye safu ya kiungo au beki wa pembeni, Kimmich alijiunga kutoka RB Leipzig mwaka 2015 na amefanikiwa kushinda mataji 17 na Bayern, ambao wanatafuta taji la 10 mfululizo la Bundesliga msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema kuwa sababu muhimu zaidi ya kuongezwa kwa mkataba wake ni kufuata mapenzi yake kwa furaha kila siku huko Bayern.
Kimmich aliongeza kuwa: “Juu ya hayo, familia yangu inahisi iko nyumbani hapa. Munich imekuwa nyumba ya pili.”
Ana taji moja la UEFA Champions League, alishinda mwaka 2020, na mataji sita ya Bundesliga mfululizo kutoka 2016 hadi 2021 na Bayern Munich.
Kimmich amefungaa mabao 30 na asisti 73 katika michezo 264 ya Bayern Munich hadi sasa.
Kiungo huyo wa ulinzi ana michezo 59 kwa timu ya taifa ya Ujerumani, akizalisha mabao matatu.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.
Sarah
Vizuri