Kwanini Messi Alistahili Ballon d'Or 2021 na Siyo Lewandowski?

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi aliibuka na ushindi wa tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka 2021 na kumpiku straika wa Bayern Munich Robert Lewandowski ambaye alishika nafasi ya pili kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kwanini Messi Alistahili Ballon d'Or 2021 na Siyo Lewandowski?

Messi ambaye amejipatia tuzo hiyo kubwa kwa mara ya 7 alifanikiwa kutwaa taji la Copa America mwaka 2021 kombe lake la kwanza kwa ngazi ya kimataifa na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo, vilevile alishinda taji la Copa del Rey akiwa na Barcelona na kumaliza mfungaji bora kwenye LaLiga msimu uliyopita.

Wakati Lewandowski alifanikiwa kufunga mabao 48 kwenye msimu wa 2020/21, hakufanikiwa kupata mafaniko na timu ya taifa kwenye michuano ya Euro 2020 pia hakufanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa na Bayern kitu ambacho kama angefanikiwa kupata mafanikio hayo basi ilikuwa ni sababu kubwa ya kuibuka mshindi wa tuzo.

Kwanini Messi Alistahili Ballon d'Or 2021 na Siyo Lewandowski?

Lewandoski alijipatia tuzo ya straika bora wa mwaka na kwa sasa ana magoli 25 kwenye michuano yote msimu huu, Msimu 2019/20 ndiyo msimu ambao Lewa alikuwa na mafanikio ambayo yange mfanya ashinde tuzo ya Ballon d’Or lakini bahati mbaya hafla hizo hazikufanyika kufuatia kuzuka kwa coronavirus.

Messi alisema wakati akipokea tuzo yake “Nataka kumwambia Lewandowski kwamba ni heshima kwangu kushindana naye kwenye tuzo hii.

“Unastahili kupata Ballon d’Or yako. Mwaka uliyopita kila mtu anakubali kwamba wewe ndiye mshindi nadhani France Football wanapaswa kukupata Ballon d’Or yako ulistahili.


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe