Mambo Manne Usiyo Yajua Kuhusu Thiago Silva.

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa mlinzi wa kimataifa Thiago Silva kutoka Brazil kwa uhamisho huru akitokea klabu ya PSG siku chache zilizopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amesaini dili ya mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele kinacho mruhusu kuongeza miezi 12 kuendelea kubaki Stamford Bridge.

Haya ni mambo manne huenda ukawa huyajui kuhusu Thiago Silva.

1.Soka lake lingeisha Mapema kutokana na maradhi.

Thiago Silva alihamia Ulaya mwaka 2004 na kujiunga na mabingwa wa Champions League kwa wakati huyo timu ya Porto.Mwaka mmoja baadaye alikwenda Dynamo Moscow lakini huko hakufanikiwa kucheza mchezo hata mmoja kwa klabu hiyo ya Urusi kutokana na kupata maumivu ya kifua na baadaye kugundilika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu, alitumia miezi isiyopungua mitano kwaajili ya tiba na kulikuwa na uwezekano wa kuondoa sehemu ya pafu lake ili kurefusha muda wa ugonjwa, hii ilikuwa ikimaanisha soka lake lingefikia tamati zamani sana.

2.Ana mpango wa kufuata nyayo za Paolo Maldini muda wa kucheza soka.

Baada ya kupona maradhi yake akiwa Brazil Thiago alianza tena kujijenga upya, mwaka 2008-09 Silva alihamia AC Milan kabla ya mkongwe Paolo Maldini haja tundika daruga na aliweza kumwambia kwamba yeye ndiyo “role model” wake na ana hamu ya kufikia mafanikio kama yake mpaka atakapo fikisha miaka 40. “Nitafuta nyayo zake mpaka pale mwili utakapo kataa,” aliongea hivyo mwaka 2016.

Mlinzi wa kati wa zamani wa AC Milan, Paolo Maldini

3.Aliwahi kutukanwa na Joey Barton

Mwaka 2013 mchezaji wa Marseille Joey Barton aliyekuwa kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea klabu ya QPR alionesha utovu wa nidhamu na baadaye kuomba radhi kwa kumuita Thiago Silva “mvulana mrembo kibonge” ishu iliyo leta mjadala mkubwa katika mtandao wa Twitter.

4.Hakuwepo kwenye mchezo Brazil ilipo pokea kichapo cha 7-1 kutoka timu ya Ujerumani.

Thiago Silva

Thiago Silva alifunga goli dhidi ya Colombia katika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 lakini baadaye alipata adhabu ya kutocheza hii ina maanisha hakuwepo kwenye mchezo ambao Brazili ilikula chuma 7-1 wakiwa mikononi mwa Wajerumani.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

50 Komentara

    Asante kwa nakala bombs kabisa pia tunamkaribisha chamani Chelsea Thiago Silva.

    Jibu

    Thnks meridian bet tz wazee wa option mwele lele za kubet na vle vle nawapa big up kwa kutupa habar za Moto ambazo hatuzifahamu thnks meridian bet tz

    Jibu

    Asanteee kwa taarifa

    Jibu

    Asanteni kwa kutujuza

    Jibu

    Asanten meridian kwa kutujuza Yale tusioyajua

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Hapa chelsea wamepata sana#Meridianbettz

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Thiago adi sasa ni Legendary

    Jibu

    Chelsea Msimu huu wamejipanga vizuri karibu thiago#meridianbett

    Jibu

    Good @meridianbettz

    Jibu

    Safi sana chelsea msimu huu mmejipanga vizuri#Meridianbettz

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    apo Chelsea wamepata jembe

    Jibu

    Safi sana thiago silva tunategemea mabadiliko huko chelsea

    Jibu

    thiago anajielewa sana na mpira anajua kuucheza ipasavyo

    Jibu

    Kila lakheri Thiago Silva kuerekea kwenye krabu mpya ya Chelsea kiungo unae jituma

    Jibu

    Amenikumbusha hayati Michael Jackson jinsi alivyoweka malengo ya kuishi miaka 150 sina kama akijitunza atacheza mpaka kufikisha miaka 40#meridianbettz

    Jibu

    Asante meridian kwa makala hii

    Jibu

    Thiago mtu hatariii!!!

    Jibu

    Thiago bengo la beki hatari

    Jibu

    Thiago beki hatar

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Beki kisiki sana.

    Jibu

    Ile mechi pengo la thigo lilionekana.

    Jibu

    Yuko vizuri bonge la mchezaji

    Jibu

    thiago namkubali sana

    Jibu

    mchezaji mzuri wame msajiri chelsea

    Jibu

    Thiago waonyeshe maajabu wazee wa darajan uwezo wako unaonekana

    Jibu

    Kwa nafax yake ya beki atachez mda mlef

    Jibu

    Axante nlkua cjui haya

    Jibu

    Nampenda sana Thiago Silva anajituma sana

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    gusd newa meridianbet

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Asante kwa habari na makala nzuri#meridianbet

    Jibu

    Thiago ni mchezaji mzuri Sana

    Jibu

    Thiago amekuja kujenga safu ya ulinzi wa Chelsea kwa uzoefu wake aliokua nao.

    Jibu

    Thiago bado yupo vizuri

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Asante kwa taarifa Meridian bet

    Jibu

    Dahh kumbe alishaumwa TB pole yake

    Jibu

    Kwa kuangalia histor yake sijui kama Chelsea wataweza kudumu naye ukiangalia uwezo wake thiago ushashuka sasa hivi ni bola wangeangalja upande mwengine tu

    Jibu

    Thiago waonyeshe maajabu wazee wa darajan uwezo wako unaonekana

    Jibu

    Waonyeshe watu waajabu

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Imekaa poa sana 👍

    Jibu

Acha ujumbe