Uchambuzi UCL Kundi E: Barcelona vs Bayern Munich

Barcelona na Bayern Munich zinaanza mbio kunako Ligi ya Mabingwa kwa mechi kali ya Kundi E huko Camp Nou siku ya Jumanne usiku mechi itakayopigwa majira ya saa nne usiku (10:00 pm).

Uchambuzi UCL Kundi E: Barcelona vs Bayern Munich

La Blaugrana ilishika nafasi ya tatu katika msimu wa La Liga wa 2020-21 ili kupata nafasi kwenye hatua ya makundi, wakati Bayern ilimaliza nafasi ya kwanza kwa kutwaa taji la Bundesliga.

Martin Braithwaite amepata jeraha la muda mrefu wiki iliyopita na ameondolewa katika mchezo huu, Ansu Fati pia ni mchezaji mwingine ambaye atakosekana kwa The Blaugrana pamoja na usajili mpya Sergio Aguero vilevile Ousmane Dembele wote wana majeraha hii itatoa nafasi kwa Luuk de Jong kucheza dhidi ya Bayern Munich.

Serge Gnabry alitolewa kwenye mchezo dhidi ya RB Leipzig wikendi iliyopita na ni kama hatocheza , Jamal Musiala na Leroy Sane wamekuwa na kiwango cha kuvutia msimu huu na watacheza pamoja na Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji.

Kingsley Coman na Corentin Toliso wote wapo nje sababu ya majeraha. Joshua Kimmich na Leon Goretzka walitawala viungo wa Barcelona mara ya mwisho kukutana na huende wakafanya hivyo hivyo kwa mchezo wa leo.

Rekodi za Kukutana:

Bayern Munich inarekodi ya kipekee kwenye kukutana kwao kwani wameshinda mara nane katika michezo 13.Barcelona wameshinda mara tatu pekee dhidi ya Bayern Munich.

UNAWEZA KUFANYA UBASHIRI WAKO HAPA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA 2021-22


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe