Uchambuzi UEFA: Liverpool vs Real Madrid

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake itapaswa kucheza kwa uwezo wao wote ili kuhakikisha wanapindua matokeo ya 3-1 dhidi ya Real Madrid katika Champions League siku ya Jumatano na kusonga hatua ya nusu fainali.

Ushindi wa Real Madrid dhidi ya Liverpool wiki iliyopita ulimaanisha The Reds watahitaji kushinda magoli yasiyopungua mawili ilikusonga mbele.

“Unapokuwa nyuma kwa 3-1 ni kama tayari umeshaaga mashindano kwa hiyo hatuna cha kupoteza tutajaribu,” alisema Klopp.

Liverpool wamefika fainali ya Champions League mara mbili wakiwa chini ya Klopp, walipoteza kwa Real Madrid 2017-18 kabla ya kuifunga Tottenham 2018-19.

Lakini Liverpool wapo nafasi ya sita katika msimamo na wameshindwa kutetea taji la Premier League msimu huu.

Lakini Liverpool wanarekodi nzuri kwenye michuano hiyo kwani walishawahi kupoteza kwa 3-0 dhidi ya Barcelona katika dimba la Camp Nou na kuibuka na ushindi wa 4-0 Anfield.

Taarifa za Timu

Liverpool inatarajia kuwa bila nahodha wao Jordan Henderson ambaye anasumbuliwa na majeraha na straika Divock Origi anasumbuliwa na jeraha la misuli, wakati mlinzi Virgil van Dijk, Joel Matip hawapo kwenye kikosi kwa muda mrefu.

Beki wa Real Madrid Lucas Vazquez anasumbuliwa na jeraha la goti baada ya kuumia kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona wikendi na hajasafiri na kikosi, Hazard yupo nje sababu ya majeraha, Raphael Varane, Sergio Ramos wamejitenga baada ya kukutwa maambukizi ya COVID-19 hivyo hajahusishwa kwenye mchezo huu.

Kikosi cha Liverpool kinachoweza kuanza: Alisson; Alexander-Arnold, Phillips, Kabak, Robertson; Fabinho, Thiago; Salah, Firmino, Mane; Jota.

Kikosi cha Real Madrid Kinachoweza Kuanza: Courtois; Odriozola, Nacho, Militão, Mendy; Casemiro, Kroos, Modric; Asensio, Benzema, Vinicius Jr.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

4 Komentara

    Tusubiri tuone kama Liverpool anaweza kumpiku Real Madrid kutokana na ushindi wa awali aliyopata dhidi ya Liverpool ambao ni 3-1

    Jibu

    Liverpool wajipange sana

    Jibu

    Uchambuzi uko vizuri

    Jibu

    Ulikuwa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe