Utatu wa Mane, Salah na Firmino (MSF) Wawatishio UCL

Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino kwa mara nyingine wameendelea kutesa kunako ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuonyesha muunganiko mzuri katika ushindi ugenini wa 5-1 wa Liverpool dhidi ya FC Porto siku ya Jumanne usiku.
Utatu wa Mane, Salah na Firmino (MSF) Wawatishio UCL
Mohamed Salah (kusoto) Roberto Firmino (katikati) Sadio Mane (kulia) wakipongeza baada ya kufunga dhidi ya Porto

Liverpool waliutumia uwanja wa Estadio dragao kama uwanja wao huku utatu unaojulikana kama MSF wakifanya uharibifu kwa timu ya Sergio Conceicao.

Kati yao wote waliweza kuzifumania nyavu za kwenye mchezo huo wa kundi B Mo Salah akiwaweka mara mbili Mane moja na Firmino akifunga mabao mawili utatu huo kwa pamoja umefunga mabao 300 kwa klabu ingawa msimu uliyopita walionekana kutofanya vyema mpaka Klopp akalazimika kumsajili Diogo Jota.

Msimu wa 2020/21, Firmino alikuwa kisumbuliwa na majeraha wakati Mane alikiri kuwa na msimu mbaya.

Wachezaji hao machachari mpaka sasa wamefunga mabao 14 kwenye michezo mitano ya Liverpool dhidi ya timu za Ureno.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

 

Acha ujumbe