Klabu ya Queens Park Rangers (QPR) wamemtangaza Michael Beale kama kocha mkuu wa klabu hiyo leo siku y jumatano na amesaini mkataba wa kuinoa klabu hiyo wa miaka mitatu.

Michael Beale alisema: “Ni vizuri kuwa hapa . Nimekuwa nikitafuta nafasi sahihi  na nadhani nimeipata sasa hapa, kwenye klabu sahihi, watu sahihi,  hamasa sahihi  na uungwaji mkono.”

Michael Beale

Michael Beale ameacha kazi ya kuwa kocha msaidizi wa Steven Gerrard kwenye klabu ya Aston Villa. Awali alifanya kazi na Gerrard kwenye klabu ya Rangers na Liverpool kabla ya kujiunga nae West Midlands.

Beale pia alitumia muda wake kufanya kazi kwenye akademi za Liverpool na Chelsea pia alifanya kazi na klabu ya Brazili Sao Paolo.

Baada ya kufanya kazi kama msaidizi wa Gerrard, Beale alisubili kwa shauku nafasi yakuwa kocha mkuu wa klabu lakini alikuwa akisubiri muda sahihi kabla ya kubeba mikoba hiyo.

QPR, kwa sasa, wameachana na kocha wao aliyemaliza muda wake Mark Warburton kufuatia kumalizika kwa simu na mkataba wake kuisha.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa