Mechi zote mbili za robo fainali baina ya Chelsea na FC Porto, Aprili 7 na Aprili 13, zitafanyika kwenye uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan linalomilikiwa na Sevilla ya Hispania.

Chelsea
Ramon Sanchez-Pizjuan

Hii ni kutokana na masharti ya usafiri katika kipindi hiki cha COVID-19 ambapo Ureno imepiga marufuku ndege kuingia nchini humo kutokea Uingereza, au ukiingia ukae karantini kwa siku 14.

Uingereza nayo imeweka masharti kwa watu kutoka Ureno kujitenga angalau siku 10, majumbani mwao (siyo katantini) wanapoingia nchini humo, japo ndege zinaruhusiwa kutua.

Masharti haya yamesababisha UEFA kwa kushirikiana na vilabu husika kutafuta uwanja mbadala, na ndipo uwanja wa Sevilla Estadio Ramon Sanchez-Pizjuan ukapatikana.

Katika hatua ya 16 bora mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Atletico Madrid, Chelsea walishindwa kwenda Hispania kutokana na masharti ya COVID-19 na kusababisha mchezo wa nyumbani wa Atletico kufanyika jijini Bucharest Romania ambapo Olivier Giroud alipiga tiktak ya karne ya 22.

Chelsea

Hata hivyo, mchezo wa pili ulifanyika Stamford Bridge kwa sababu Uingereza haikuwa na masharti magumu kwa wasafiri kutoka Hispania.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Chelsea, Chelsea Vs FC Porto Kupigwa Ramon Sanchez-Pizjuan, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa